Wizara ya mambo ya nje ya China yaitaka Canada kuheshimu mamlaka ya sheria ya China
2021-08-13 11:04:26| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi Hua Chunying amezitaka nchi husika kuheshimu mamlaka ya kisheria ya China na kuacha kutoa hoja zisizowajibika.

Agosti 10 na 11, mahakama za mkoa wa Liaoning na mji wa Dandong zilitoa hukumu kwa nyakati tofauti kuhusu kesi za raia wa Canada Robert Lloyd Schellenberg na Michael Spavor. Upande wa Canada umetoa taarifa ikiilaumu hukumu dhidi ya wahalifu hao wawili na kudai itaendelea kutafuta njia za kuachiwa kwa watu hao. Umoja wa Ulaya na Uingereza pia zimetoa sauti kuiunga mkono Canada.

Bi. Hua amesema China inalaani vikali Canada kushirikisha nchi kadhaa kuingilia hukumu ya mahakama husika dhidi ya kesi za raia wa Canada nchini China, njia hiyo imekiuka vibaya mamlaka ya sheria ya China na msingi wa utawala wa kisheria.

Amesema mtuhumiwa Schellenberg alishiriki kwenye magendo ya dawa za kulevya ya kuvuka mipaka, huku Michael ameshtakiwa kutokana na uhalifu unaodhuru usalama wa taifa wa China. Mahakama husika zimetoa hukumu hadharani kwenye msingi wa kuthibitisha uhalifu wa watuhumiwa hao, na haki halali za watu hao wawili zimehakikishwa kikamilifu.