Balozi wa China nchini Marekani aelezea msimamo wa China juu ya suala la Taiwan kwa Marekani
2021-08-13 09:21:08| cri

Balozi wa China nchini Marekani Bw. Qin Gang na Naibu waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bibi Wendy Sherman walikutana tarehe 12 mwezi huu na kubadilishana maoni kwa kina kuhusu masuala wanayoyafuatilia kwa pamoja.

Bibi Sherman alimkaribisha balozi Qin Gang kuanza kazi yake nchini Marekani na kusema Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani itatoa ushirikiano ili kurahisisha kazi yake. Balozi Qin Gang amemshukuru Bibi Wendy na kusema ataendelea kuhimiza uhusiano wenye busara wa kiujenzi kati ya nchi hizo mbili.

Balozi Qin alipozungumza na wanahabari baada ya mkutano, alisema pande zote mbili zimekubalina kuwa uhusiano kati ya nchi zao ni muhimu sana, na zitatatua masuala mbalimbali kupitia mazungumzo na mawasiliano ili kuboresha uhusiano huo. Pia amesisitiza kuwa amemweleza wazi Bibi Sherman msimamo wa China juu ya suala la Taiwan, ambalo ni suala nyeti na muhimu zaidi kwenye uhusiano kati ya China na Marekani.