Shehena ya tatu ya chanjo ya COVID-19 kutoka China yawasili Iraq
2021-08-13 09:17:49| CRI

Shehena ya tatu ya chanjo ya COVID-19 iliyotolewa kama msaada na serikali ya China imewasili Baghdad nchini Iraq. Wawakilishi kutoka wizara ya afya ya Iraq na ubalozi wa China nchini Iraq walihudhuria hafla ya kupokea shehena hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.

Kaimu balozi wa China nchini Iraq Bw. Jian Fangning, alisema China na Iraq ni marafiki wakubwa na washirika wazuri. Baada ya kutokea kwa janga la Covid-19, China na Iraq zilishirikiana kupambana na janga hilo, na amesema anaamini kuwa shehena hiyo itaisaidia Iraq kujenga kinga dhidi ya janga hilo.