Taliban yaingia mjini Kabul
2021-08-16 07:52:27| CRI

 

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Juu ya Mapatano ya Taifa ya Afghanistan Abdullah Abdullah said amesema, rais Mohammad Ashraf Ghani wa nchi hiyo ameondoka kutoka kwenye nchi hiyo. Kabla ya hapo, msemaji wa Kundi la Taliban amesema wapiganaji wa kundi hilo wameingia mjini Kabul.

Habari zinasema Ghani amekubali kujiuzulu, na amekwenda nchini Tajikistan pamoja na maofisa wengine wa serikali ya Afghanistan.

Msemaji wa Taliban Zabiullah Mujahid amesema kutokana na vikosi vya usalama vya serikali kuacha jukumu la kulinda usalama mjini Kabul, wapiganaji wa kundi hilo limeingia mjini humo, ili kuhakikisha usalama wa watu na utaratibu wa jamii.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia msemaji wake amesema anafutalia hali nchini Afghanistan, na kuhimiza Taliban na pande nyingine kujizuia kadiri ziwezavyo, ili kuhakikisha usalama wa maisha ya watu na mahitaji ya kibinadamu.