Sudan yarejea ahadi yake ya kuzuia hali kuwa mbaya zaidi nchini Ethiopia
2021-08-16 08:33:51| CRI

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok amerejea tena ahadi ya nchi yake ya kujitahidi kadri inavyoweza kuzuia hali nchini Ethiopia kuwa mbaya zaidi.

Akizungumza na wanahabari mjini Khartoum, Bw. Hamdok amesema, ndani ya mfumo wa Shirika la Maendeleo la Kiserikali la Nchi za Afrika Mashariki (IGAD), amewasiliana na viongozi wa nchi wanachama wa kundi hilo na wa kanda na nchi za kigeni kutafuta suluhisho la mgogoro unaoendelea katika mkoa wa Tigray nchini Ethiopia.