Idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi magharibi mwa Haiti yafikia 724
2021-08-16 08:37:10| cri

Idara ya Ulinzi ya Raia nchini Haiti imesema, mpaka kufikia jana mchana, idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.2 kwenye kipimo cha Richter lililotokea jumamosi magharibi mwa nchi hiyo, imefikia 724.

Mkuu wa idara hiyo Bw. Jerry Chandler amesema, tetemeko hilo pia limesababisha majeruhi 2,800, na waathiriwa wengi wanatokea mkoa wa kusini magharibi mwa nchi hiyo

Waziri Mkuu wa Haiti, Bw. Ariel Henry, amefika katika eneo la tukio na kuelekeza kazi za uokoaji, pia ametangaza kuwa, kufuatia tetemeko hilo,  Haiti imeanza kipindi cha dharura kwa mwezi mmoja.