Rais wa China ampongeza mwenzake wa Korea Kusini katika maadhimisho ya miaka 73 ya Siku ya Ukombozi wa nchi hiyo
2021-08-16 08:38:03| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana Agosti 15 amemwandikia barua ya pongezi mwenzake wa Korea Kusini Moon Jae-in katika maadhimisho ya miaka 73 ya Siku ya Ukombozi wa nchi hiyo.

Katika barua hiyo, Rais Xi amesema, China na Korea Kusini ni nchi jirani muhimu, na uhusiano kati yao umeendelezwa vizuri katika miaka ya karibuni. Amesema tangu janga la COVID-19 lilipotokea, nchi hizo mbili zimesaidiana na kushirikiana kupambana na janga hilo, kuongoza mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali kupata matokeo mapya, na kuonyesha kiwango cha juu cha uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakati kati yao.

Rais Xi amesema, China siku zote inazingatia kuendeleza uhusiano kati yake na Korea Kusini, na anapenda kuimarisha mawasiliano ya kimkakati kati yake na rais Moon Jae-in. Pia kuinua uhusiano kati ya China na Korea Kusini kufikia kiwango cha juu zaidi, kunufaisha nchi hizo mbili na wananchi wao, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya amani, utulivu na ustawi wa kikanda.