Cote d'Ivoire yathibitisha kesi ya kwanza ya Ebola
2021-08-16 09:51:21| CRI

 

 

Waziri wa Afya, Afya ya Umma na Bima ya Tiba kwa Wote wa Côte d'Ivoire Bw. Pierre Dimba, amesema kupitia televisheni kuwa, kesi ya Ebola imethibitishwa Abidjan, mji mkuu wa uchumi wa nchi hiyo.

Waziri huyo amesema, mtu aliyethibitishwa kuwa na virusi vya Ebola ni msichana mwenye umri wa miaka 18, ambaye aliwasili Abidjan kwa barabara akitokea mji wa Rabe nchini Guinea tarehe 11 mwezi huu, na tarehe 14 alithibitishwa kuwa na virusi vya Ebola. Hivi sasa mgonjwa huyo amewekwa karantani katika Kituo cha Matibabu ya Magonjwa ya Kuambukiza cha Trecheville mjini Abidjan.

Serikali ya Côte d'Ivoire iliwataka raia wasiwe na hofu, na kusema itatoa chanjo dhidi ya Ebola wafanyakazi wa matibabu walio mstari wa mbele, watu waliowasiliana karibu na mgonjwa na walinzi usalama wa mipakani, pia itafanya kazi ya ufuatiliaji wa janga pamoja na Guinea.

      Mlipuko wa Ebola ulitokea Guinea tarehe 14 mwezi Februari mwaka huu.