Wahadhiri nchini Kenya waanza mafunzo ya teknolojia ya juu yanayotolewa na kampuni ya Huawei
2021-08-17 08:25:15| CRI

Wahadhiri kutoka vyuo vya elimu na ufundi stadi nchini Kenya (KVET) wameanza mafunzo yanayofadhiliwa na kampuni ya mawasiliano ya China, Huawei, ili kuongeza ujuzi wao katika teknolojia ya juu.

Katika taarifa yake iliyotolewa jijini Nairobi, Huawei imesema wahadhiri hao wamepata mafunzo kuhusu usalama, ambao ni muhimu katika kulinda miundombinu ya kidijitali inayokua kwa kasi nchini Kenya. Kampuni hiyo imesema, wahadhiri waliopata mafunzo hayo wanatarajiwa kuhamisha ujuzi huo kwa wanafunzi zaidi ya elfu moja na kuwaandaa kwa ajili ya Mageuzi ya Nne ya Kiviwanda.

Mpaka sasa, Huawei imetoa mafunzo kwa wahadhiri 51 kutoka vyuo vikuu, vyuo vya ufundi stadi na vyuo vya elimu nchini Kenya chini ya program ya TEHAMA.