Idadi ya watu waliofariki katika tetemeko la ardhi nchini Haiti yafikia 1,419
2021-08-17 08:24:16| CRI

Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea kusini magharibi mwa Haiti jumamosi imeongezeka na kufikia 1,419, na watu wengine 6,900 kujeruhiwa.

Mamlaka ya ulinzi wa raia nchini humo imesema, tetemeko hilo pia limesababisha uharibifu wa nyumba zaidi ya 37,000.

Akizungumza na wanahabari, mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Jerry Chandler amesema jamii ya kimataifa inaendelea kuiunga mkono Haiti katika kukabiliana na janga hilo.