Uwekezaji wa kigeni nchini China katika miezi 7 iliyopita waongezeka kwa asilimia 25 kuliko mwaka jana
2021-08-17 08:07:13| CRI

Takwimu kutoka wizara ya biashara ya China zinaonyesha kuwa, kuanzia mwezi Januari hadi mwezi Julai mwaka huu, uwekezaji wa kigeni nchini China umefikia dola za kimarekani bilioni 103, ikiwa ni ongezeko la asilimia 25 kuliko mwaka jana wakati kama huo.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, katika kipindi hicho, sekta ya huduma imepata uwekezaji zaidi ya dola za kimarekani bilioni 82.6, ikiongezeka kwa asilimia 29.2 kuliko mwaka jana wakati kama huo. Uwekezaji kutoka nchi za “Ukanda mmoja, Njia moja” na nchi za Umoja wa Asia Kusini Mashariki umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 46 kuliko mwaka jana wakati kama huo.