Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa aonya dhidi ya Afghanistan kurudi tena kuwa maficho ya magaidi
2021-08-17 14:37:40| Cri

Naibu mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Geng Shuang jana alitahadharisha kuhusu Afghanistan kurudi tena kuwa maficho ya magaidi. Amekumbusha kuwa miaka 20 iliyopita, makundi ya kigaidi kama IS, kundi la al-Qaida na kundi la harakati ya uhuru wa Turkistan Mashariki yalijikusanya na kuitumia Afghanistan kama kituo chao, na kutishia amani na usalama wa kikanda na kimataifa.

Alisema katika mkutano wa dharura wa baraza la usalama kuhusu hali ya Afghanistan kwamba Afghanistan haipaswi kuwa kituo cha ugaidi tena. Huu ndio msingi wa mpango wowote wa kisiasa wa Afghanistan.