Hatua inayofuata ya kutafuta chanzo cha virusi vya COVID-19 lazima iongozwe na nchi wanachama wa WHO
2021-08-17 10:29:11| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, kazi ya kutafuta chimbuko la virusi vya Corona ni muhimu, na inapaswa kuongozwa na nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Habari zinasema, Sekretarieti ya WHO ilitoa taarifa kuwa, hatua ijayo inapaswa kutegemea utafiti wa kipindi cha kwanza na kutekeleza mapendekezo katika ripoti ya pamoja ya utafiti wa China na WHO,  na inasema uchunguzi juu ya chimbuko la virusi vipya unapaswa kutegemea misingi ya kisayansi na sio kugeuzwa na kuwa silaha za kisiasa.