Wakazi wa Mukuru kuanza kununua maji kwa kutumia tokeni
2021-08-17 07:56:53| cri

Huduma za mjini  (NMS) na Kampuni ya Maji na Maji taka ya Jiji la Nairobi zinatarajiwa kuanzisha mfumo wa tokeni za maji katika vitongoji duni vya Mukuru vya Nairobi ambavyo vitaona mtungi wa lita 20 akiuzwa kwa senti 50.

Tayari, vituo 10 ambavyo vitatumia mfumo huu vimeanzishwa katika maeneo ya kimkakati katika makazi duni na wakazi wa Mukuru kwa Reuben wanaotarajiwa kuwa walengwa wa kwanza wa mradi huo.

Naibu Mkurugenzi wa NMS wa Maji na Usafi wa Mazingira Stephen Githinji amesema mradi huo unakusudia kuimarisha upatikanaji wa maji safi kwa bei rahisi kwa wakazi wa eneo lenye kipato cha chini.

Wachuuzi wa maji wametengeneza pesa katika shida iliyopo sasa ya maji  ambapo wanauza mtungi wa lita 20 kati ya Sh20 na Sh50.