China yasema Reli ya Addis Ababa-Djibouti inachochea maendeleo ya uchumi wa Ethiopia na Djibouti
2024-05-15 09:25:18| CRI

Mkutano wa kutangaza matokeo ya miaka sita iliyopita na mtazamo wa siku za usoni kuhusu Reli ya Addis Ababa-Djibouti ambao pia ni hafla ya kukabidhi ufunguo ulifanyika hivi karibuni mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin tarehe 14 alisema Reli ya Addis Ababa-Djibouti ni mradi wa kujenga kwa pamoja pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kati ya China na Ethiopia na Djibouti, ambayo inawapatia watu wa huko zaidi ya elfu 55 nafasi za ajira tangu ilipomalizika kujengwa, pia inachochea zaidi maendeleo ya uchumi wa Ethiopia na Djibouti.

Ameongeza kuwa hafla hiyo inamaanisha kuwa huduma ya uendeshaji na matengenezo ya upande wa China kwa reli hiyo imemalizika, na sasa upande wa Afrika unaendesha reli hiyo kikamilifu. China itaendelea kushirikiana na Ethiopia na Djibouti, na kuifanya reli hiyo iwe njia yenye ustawi katika kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana.