Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa latoa wito wa kusitisha vurugu na kuunda serikali ya umoja nchini Afghanistan
2021-08-17 08:24:42| CRI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito wa kusimamishwa mara moja kwa vurugu nchini Afghanistan na kuanzisha serikali mpya ya umoja, jumuishi na uwakilishi, ikiwa ni pamoja na ushirikishwaji kamili na wa usawa kwa wanawake.

Katika taarifa yake, Baraza hilo limesema, ni lazima Afghanistan ihakikishe inaendeleza taasisi zilizopo na kutimiza wajibu wake wa kimataifa, pamoja na kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia wote wa Afghanistan na wa kigeni.

Wakati huohuo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying amesema, China inaheshimu maamuzi ya watu wa Afghanistan, na inatumai kuwa mabadiliko ya nchini humo yatafanyika kwa amani. Amesema China inatumai kuwa kundi la Taliban litatimiza ahadi zake na kuzuia vitendo vyote vya kigaidi na kihalifu, kuwalinda wananchi wa Afghanistan na vita, na kufanya ukarabati wa nchi hiyo.