Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Marekani wazungumza kwa njia ya simu
2021-08-17 08:58:00| CRI

 

 

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amezungumza na mwenzake wa Marekani Antony Blinken kwa njia ya simu, na kubadilishana maoni kuhusu masuala mbalimbali haswa uhusiano wa nchi hizo na hali ya Afghanistan.

Wang amesema, China na Marekani zote ni nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, pia ni washiriki muhimu wa mfumo wa kimataifa, hivyo zinapaswa kufanya uratibu na ushirikiano.

Kuhusu suala la Afghanistan, Wang amefafanua msimamo wa China, na kusema ukweli umethibitisha tena kuwa kuhamisha mfumo wa kisiasa kwa nchi yenye historia na tamaduni tofauti sana hakutashinda. Amesema China inapenda kudumisha mawasiliano na mazungumzo na Marekani, ili kuhimiza Afghanistan kujenga muundo wa kisiasa unaoendana na hali halisi ya nchi hiyo.

Kwa upande wake, Blinken amesema Marekani na China kudumisha mawasiliano kuhusu msuala muhimu ya kikanda na kimataifa ni muhimu sana, na nchi hizo mbili kuishi pamoja kwa amani ni lengo lao la pamoja.