Wanasayansi wa Afrika wapendekeza kubadilisha sera ili kufikia malengo ya anuwai ya viumbe
2021-08-18 11:10:55| Cri

Wanasayansi wa Afrika jana walisema huko Nairobi kwamba kufikia malengo ya kurudisha anuwai ya viumbe iliyotolewa na jamii ya kimataifa, serikali na wafadhili kutategemea mageuzi ya sera, ufadhili wa kutosha na ushiriki mkubwa wa jamii.

Kulingana na utafiti uliopewa jina la “kuunganisha malengo ya anuwai ya viumbe kutoka viwango vya ndani hadi vya nje”, inahitaji kuunda tena sera na sheria inayosimamia uhifadhi wa makazi na kuhakikisha zinawahusu watu na ni shirikishi.