Chombo cha kuchunguza sayari ya Mars cha China chamaliza kazi yake kilizopangiwa
2021-08-18 11:35:42| Cri

Chombo cha kuchunguza sayari ya Mars cha China Zhurong kimemaliza kazi yake ya uchunguzi na ugunduzi kama ilivyopangwa kwa mujibu wa Shirika la Safari za Anga ya Juu la China (CNSA) Jumanne wiki hii.

Hadi kufikia Agosti 15, Zhurong imefanya kazi kwenye Mars kwa karibu siku 92 na kusafiri mita 889 kwenye sayari hiyo ambapo imekusanya takwimu mpya karibu Gb 10. Sasa chombo hicho kinaendeshwa vizuri kikiwa na nishati ya kutosha.

CNSA iliongeza kuwa chombo hicho kitaendelea kuelekea eneo la mipakani kati ya bahari ya kale na ardhi ya kale katika sehemu ya kusini ya Utopia Planitia na kuendelea na kazi nyingine.

Limesema Zhurong ilifanya kazi kwa mzunguko wa siku saba wakati wa uchunguzi na ugunduzi wake. Kamera yake ilipata data ya hali ya juu njiani ambazo zinaweza kusaidia kigari hicho kupanga njia yake na kuchagua shabaha ya kuchunguzwa.