China yatarajia utawala mpya wa Afghanistan uvunje na uhusiano na kundi la magaidi
2021-08-18 11:10:25| Cri

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying jana alisema kwamba China inauhimiza upande wa Taliban nchini Afghanistan kutekeleza sera ya wastani ya kidini, ikiitaka serikali mpya ya Afghanistan ikate uhusiano wa kila aina na makundi ya kigaidi ya kimataifa.

Aidha Bibi Hua amesema China inatumai kuwa upande wa Taliban utashirikiana na pande zote katika kuanzisha mfumo wazi na shirikishi wa kisiasa, na kutekeleza sera yenye amani na urafiki ya kidiplomasia, haswa kuendeleza uhusiano wa kirafiki na nchi jirani, ili kutimiza ukarabati na maendeleo nchini Afghanistan.

Alisema serikali mpya ya Afghanistan inapaswa kupinga makundi ya kigaidi likiwemo kundi la harakati ya Kiislamu la Turkestan Mashariki, ili kuizuia Afghanistankuwa tena mahali pa kukusanyika makundi ya kigaidi na yenye msimamo mkali.