Rais wa China asisitiza kuhimiza ustawi wa pamoja na maendeleo ya hali ya juu kwa kukinga hatari kubwa ya kifedha
2021-08-18 11:35:16| Cri

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuimarisha juhudi za kuhimiza ustawi wa pamoja katika kutafuta maendeleo ya hali ya juu na kuratibu kazi husika kwa kukinga hatari kubwa ya kifedha na kuzingatia falsafa ya maendeleo yanayolenga watu wake kwani ustawi wa pamoja ni sharti la kimsingi la ujamaa na sifa kuu ya maendeleo ya kisasa yenye umaalumu wa kichina.

 

Rais Xi alibainisha kuwa mambo ya kifedha ndio msingi wa uchumi wa kisasa na juhudi za kukinga hatari kubwa za kifedha zinapaswa kuratibiwa kulingana na kanuni za soko na sheria.

Imesisitiza kwamba wakati China inapoelekea kutimiza lengo lake la karne ya pili, kiini cha kuhimiza ustawi wa watu kinapaswa kuzingatia ustawi wa pamoja ili kuimarisha msingi wa utawala wa muda mrefu wa Chama cha Kikomunisti cha China.

Ustawi ya pamoja ni ustawi unaoshirikiwa na kila mtu wa nchi katika sekta za kiuchumi na kitamaduni na ungesongeshwa mbele hatua kwa hatua.