Mapato ya wastani yanayotumika ya kila mtu kwa wakazi wa vijijini mkoani Tibet yaongezeka kwa asilimia 12.5
2021-08-18 08:45:11| cri

 

 

Makamu wa mwenyekiti mtendaji wa Serikali ya Mkoa unaojiendesha wa Tibet, jana kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema tangu mkutano wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ulipofanyika, idadi ya watu maskini vijijini mkoani Tibet imepungua kwa 850,000, na idadi hiyo inapungua kwa watu 106,000 kwa wastani wa mwaka. Kuanzia mwaka 2012 hadi 2020, mapato ya kila mtu kwa wakazi wa vijijini huko Tibet yameongezeka kutoka Yuan 5,698 hadi Yuan 14,598, ongezeko la wastani kwa mwaka ni 12.5%.

Tangu mapambano dhidi ya umaskini yaanze, Tibet imechukua uendelezaji wa viwanda kama msingi wa kuondoa umaskini, na wakati huo huo, imechukua hatua nyingi za kuwasaidia watu kuondokana na umaskini, ikiwa ni pamoja na kubadilisha ajira, kuwahamishia watu sehemu nyingine ili kuondokana na umaskini, kuondokana umaskini kwa kuhimiza uhifadhi wa kibailojia, kuongeza utoaji wa elimu, na kuweka kigezo cha msingi cha maisha.