Rais wa China atoa barua ya pongezi kwa Maonyesho ya Tano ya Biashara kati ya China na Nchi za Kiarabu
2021-08-19 11:41:56| Cri

Rais Xi Jinping wa China ametoa barua ya pongezi tarehe 19 mwezi Agosti kwa Maonyesho ya Tano ya Biashara kati ya China na Nchi za Kiarabu yaliyofanyika huko mji wa Yinchuan, mkoani Ningxia.

 

Kwenye barua hiyo, rais Xi ameeleza kwamba, urafiki wa jadi kati ya Wachina na Waarabu umeimarishwa na kwenda na wakati. Katika miaka ya hivi karibuni, China na nchi za Kiarabu zimeendelea kuimarisha uratibu na upatanisho kati ya pande hizo mbili huku ujenzi wa pamoja wa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja” ukipata matokeo mazuri. China imeendelea kuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa nchi za Kiarabu. Na China na nchi za Kiarabu zinashirikiana katika kukabiliana na janga la virusi vya Corona ambayo imetoa mfano mzuri wa kusaidiana.

 

Rais Xi Jinping alisisitiza kuwa China inapendelea kushirikiana na nchi za Kiarabu kutafuta ushirikiano na maendeleo, kukuza maendeleo ya amani, kupata faida ya pamoja, kuhimiza ujenzi wa hali ya juu wa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kuinua ushirikiano katika kiwango cha juu na kujenga mustakbali mzuri wa pamoja katika enzi mpya.