Rais wa Afghanistan aunga mkono kundi la Taliban kufanya mazungumzo na maofisa wa zamani wa serikali
2021-08-19 08:41:33| cri

Rais Mohammad Ashraf Ghani wa Afghanistan amesema sasa yuko nchini Falme za Kiarabu na anaunga mkono mazungumzo kati ya kundi la Taliban na maofisa wa zamani wa serikali ya Afghanistan akiwemo aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hamid Karzai.

Bw. Ghani alisema alilazimika kuondoka Afghanistan ili kuepusha migogoro na janga kubwa zaidi. Wakati huo huo amekanusha shutuma kuwa alibeba pesa nyingi alipoondoka nchi hiyo.

Hivi sasa Bw. Ghani anafanya mazungumzo na pande husika kuhusu kurudi Afghanistan ili kuendelea kuwahudumia watu wa Afghanistan.