Matumizi ya teknolojia mpya katika ulinzi wa amani wa UM yapaswa kuheshimu mamlaka ya nchi zinazowakaribisha
2021-08-19 11:19:51| Cri

Naibu mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing jana alisema kwamba matumizi ya teknolojia mpya katika ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa yanapaswa kuheshimu mamlaka na matarajio ya nchi zinazowakaribisha.

Balozi Dai Bing alisema kuwa, ujumbe wa kulinda amani unapaswa kufanya majadiliano na nchi hizo wakati wanapotumia teknolojia za kufanya upelelezi na ufuatiliaji ili kuhakikisha kuwa matumizi ya teknolojia husika yanaheshimu mamlaka zao na kulinda kanuni ya Umoja wa Mataifa, pamoja na kanuni ya kutoingilia mambo ya ndani ya nchi hizo, na kufuata kanuni za kimsingi za kulinda amani.