Rais Xi Jinping wa China amesema kuwa China inaona umuhimu mkubwa kuendeleza uhusiano na Iraq, na iko tayari kukuza ushirikiano wao wa kimkakati kwa maendeleo zaidi.
Katika mazungumzo yao kwa njia ya simu na mwenzake wa Iraq Barham Salih, rais Xi alisema China iko tayari kuendelea kuunga mkono mapambano ya Iraq dhidi ya janga la COVID-19, kupanua ushirikiano wa pande mbili katika nyanja za nishati, umeme na usafirishaji, na kusaidia Iraq kujenga uchumi na maendeleo ya kijamii.
Aidha rais Xi Jinping wa China alisema kuwa China iko tayari kushirikiana na Iran katika kuhimiza maendeleo thabiti na endelevu ya ushirikiano wao kamili wa kimkakati..
Rais Xi ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Iran miaka 50 iliyopita, uhusiano wa nchi mbili umeshinda majaribu ya mabadiliko ya kimataifa, na urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili unazidi kuimarika.
Wakati zikishirikiana pamoja dhidi ya COVID-19, nchi hizo mbili zimeimarisha mshikamano na uratibu, zimepata maendeleo mazuri katika ushirikiano wa vitendo, zimeimarisha ufanisi wa kuaminiana kimkakati, na zimetetea kabisa haki ya kimataifa.