Rais wa China azungumza na wenzake wa Iran na Iraq kwa njia ya simu
2021-08-19 08:29:34| CRI

 

 

Rais Xi Jinping wa China jana kwa nyakati tofauti alizungumza kwa njia ya simu na rais Ebrahim Raisi wa Iran na rais Barham Salih wa Iraq.

Alipozungumza na rais Raisi amesema, katika miaka 50 iliyopita tangu China na Iran zianzishe uhusiano wa kibalozi, nchi hizo zimeshirikiana na kusaidiana vizuri, China inaipongeza Iran kwa kuendeleza uhusiano kati yao kwa hatua madhubuti, na kupenda kushirikiana nayo kuhimiza uhusiano wao kupata maendeleo zaidi.

Rais Raisi amesema serikali ya Iran imetoa kipaumbele katika kuendeleza uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati yake na China, Iran inaishukuru China kwa kuisaidia kukabiliana na janga la COVID-19, na kuwa na msimamo wa haki katika mambo ya kikanda na kimataifa yanayohusika na Iran.

Alipozungumza na rais Barham Salih, rais Xi amesema Iraq ni mwenzi muhimu wa China katika ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na China ikiwa rafiki wa dhati wa Wairaq, imeshiriki  kwenye ukarabati wa Iraq kwa hatua madhubuti, na kusukuma mbele ushirikiano na Iraq katika sekta mbalimbali.

Rais Barham amesema nchi yake inapenda kukuza uhusiano wa kirafiki na China, na kupanua ushirikiano katika sekta za utamaduni, utalii, vijana, michezo na kupambana na janga la COVID-19.