Kenya yaimarisha hatua za vizuizi vya COVID-19 kutokana na ongezeko la maambukizi
2021-08-19 08:05:34| CRI

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kuongeza siku 60 zaidi za marufuku ya kutotoka nje usiku na mikusanyiko ya umma, kutokana na kuongezeka kwa wasiwasi wa maambukizi ya virusi vya COVID-19 aina ya Delta.

Rais Kenyatta amesema katika taarifa iliyotolewa mjini Mombasa kuwa hatua zinazotoana na tishio la shinikizo kwenye mfumo wa afya ya umma wa Kenya. Rais Kenyatta amesema kuna ongezeko kubwa la maambukizi katika nchi nzima, ambalo linatokana na mikusanyiko isiyodhibitiwa na kupuuza miongozo ya afya ya umma.

Rais Kenyatta amesema muda wa kutotoka nje usiku unaoanza kutoka saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri, na kuzuia aina zote za mikusanyiko ya umma kwa miezi miwili, kutasaidia kudhibiti maambukizi wakati Kenya inakabiliana na wimbi la nne. Mikusanyiko kama harusi na mazishi itadhibitiwa kuwa na watu 100, ili kuepusha mikusanyiko kama hiyo kueneza maambukizi kwa wingi.