Watu 47 wafariki dunia kwenye ajali ya boti kwenye pwani ya bahari ya Atlantiki ya Afrika Kaskazini
2021-08-19 08:21:17| cri

Habari iliyotolewa jana kwa pamoja na Shirika la wahamiaji Duniani (IOM) na Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), imesema watu 47 wamefariki dunia katika ajali ya boti iliyotokea katika pwani ya bahari ya Atlantiki ya Afrika Kaskazini hadi Visiwa vya Canary vya Hispania.

Kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, boti hiyo iliyokuwa imebeba watu 54 wakiwemo watoto watatu, iliondoka tarehe 3 mwezi Agosti. Baada ya siku mbili baharini, hitilafu ya injini iliwafanya abiria wakwame bila chakula na maji kwa karibu wiki mbili.

Habari hiyo imesema, tarehe 16 mwezi Agosti mlinzi wa pwani ya Mauritania aliigundua boti hiyo ikiwa na watu saba wakiwa hai.