Askari 11 wa jeshi la Mali wauawa kwenye shambulizi katikati mwa nchi hiyo
2021-08-20 08:19:13| cri

Jeshi la Mali limesema askari 11 wameuawa kwenye shambulizi lililotokea kwenye eneo la katikati mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa jeshi la Mali, kikosi cha askari jana mchana kilishambuliwa kwenye eneo la Mopti, kwa mabomu ya kutengwa kwenye gari, halafu kimeshambuliwa na watu wenye silaha wasiojulikana. Shambulizi hilo limesababisha vifo vya askari 11 na wengine 10 kujeruhiwa.

Hadi sasa bado hakuna kundi lolote au mtu binafsi aliyetangaza kuwajibika na shambulizi hilo.