Watu wanne wameuawa kwenye mlipuko wa bomu la kujitoa muhanga mjini Mogadishu
2021-08-20 08:28:17| CRI

Watu wanne wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu la kujitoa mhanga uliotokea jana mjini Mogadishu.

Ofisa mmoja wa polisi amesema mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliingia kwenye mgahawa uliokuwa na pilika nyingi karibu na makutano ya Juba na kujilipua, na kusababisha majeruhi wengi. Hadi sasa ni watu wanne ikiwa ni pamoja na mshambuliaji wa kujitoa mhanga wamethibitishwa kuuawa, na wengine wengi wamejeruhiwa

Eneo lilipotokea shambulizi hilo ni karibu na makao makuu ya Idara ya ujasusi ya taifa (NISA) na mgahawa huo hutembelewa mara kwa mara na wafanyakazi wa idara hiyo. Hata hivyo bado haijaelezwa kama maofisa wa usalama ni miongoni mwa majeruhi kwenye mlipuko huo.

Kwa sasa vikosi vya usalama vimezingira eneo la tukio.