Uwekezaji wa China katika nchi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja” waendelea kuongezeka katika miezi 7 ya mwaka huu
2021-08-20 08:07:15| CRI

Takwimu kutoka wizara ya biashara ya China zinaonyesha kuwa, katika kipindi cha Januari hadi Julai mwaka huu uwekezaji wa moja kwa moja wa China kwa nchi za nje umefikia dola za kimarekani bilioni 62.6, ukipungua kwa asilimia 4 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho. Thamani ya miradi ya kandarasi katika nchi za nje imefikia dola za kimarekani bilioni 78.52, ikiongezeka kwa asilimia 3.4 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho.

Msemaji wa wizara hiyo Bw. Gao Feng, amesema katika miezi saba ya kwanza ya mwaka huu, uwekezaji wa China kwa nchi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja” umeendelea kuongezeka, na soko la miradi ya kandarasi limekuwa tulivu.