Maonesho ya 5 ya China na nchi za Kiarabu yafunguliwa
2021-08-20 09:22:13| CRI

 

 

Maonesho ya 5 ya China na nchi za Kiarabu yenye kauli mbiu ya  kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, na kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja” yamefunguliwa mjini Yinchuan kaskazini magharibi mwa China.

Kwenye ufunguzi wa maonesho hayo, naibu mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Shao Hong, amesema kwa kufuata kanuni ya kujadiliana, kujenga kwa pamoja na kunufaika kwa pamoja, China na nchi za Kiarabu zitashirikiana na kusaidiana ili kupata mafanikio ya pamoja.

Ikiwa ni jukwaa la ushirikiano na mawasiliano kati ya China na nchi za Kiarabu, maonesho hayo yamefanyika kwa awamu 4, na kushirikisha nchi 112, viongozi 21, mawaziri 283, zaidi ya kampuni 5,000 na zaidi ya watu elfu 40.

Mwaka jana thamani ya biashara kati ya China na nchi za Kiarabu ilifikia dola bilioni 239.4 za Kimarekani, na China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa nchi za Kiarabu.