Reli ya kisasa ya Kenya yasafirisha tani milioni 2.31 za mizigo kuanzia mwezi Januari hadi Mei
2021-08-20 10:48:35| Cri

Kulingana na takwimu zilizotolewa na Shirika la Reli la Kenya, treni ya mizigo ya SGR ya Kenya imesafirisha tani milioni 2.31 za mizigo katika miezi mitano ya kwanza mwaka huu, likiwa ni ongezeko la asilimia 45 kuliko kipindi kama hicho cha mwaka 2020. Ongezeko hilo linaonyesha mahitaji ya huduma ambayo imeongeza ufanisi katika usafirishaji wa mizigo.

Aidha idadi ya abiria wanaotumia treni katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2021 iliongezeka mara mbili wakati wa janga la COVID-19.