Idadi ya watu waliofariki kwenye tetemeko la ardhi la Haiti yaongezeka na kufikia 2,207
2021-08-23 11:53:20| CRI

Idadi ya watu waliofariki kwenye tetemeko la ardhi la Haiti yaongezeka na kufikia 2,207

Shirika la ulinzi wa raia la Haiti limesema, idadi ya watu waliofariki kwenye tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.2 kwenye kipimo cha richter ambalo lilitokea Agosti 14 imeongezeka na kufikia 2,207, huku watu wengine 344 wakiwa bado hawajapatikana.

Kwenye twitter yake shirika hilo limesema kwamba wiki moja baada ya tetemeko la ardhi ambalo pia limesababisha majeruhi ya watu 12,268, idadi ya nyumba zilizoharibika imepindukia 77,000, huku karibu 53,000 zikiteketezwa.

Kitovu cha tetemeko hilo la ardhi kilikuwa kilomita 25 magharibi mwa Port-au-Prince na lilikuwa na kina cha kilomita 10, ndio maana wakati huo ilitolewa tahadhari ya tsunami, lakini baadaye iliondolewa.