Msemaji wa Taliban asema masuala ya kuunda serikali mpya yanatarajiwa kutangazwa hivi karibuni
2021-08-23 11:44:04| CRI

Msemaji wa Taliban asema masuala ya kuunda serikali mpya yanatarajiwa kutangazwa hivi karibuni_fororder_1

Habari kutoka televisheni ya TOLO ya Afghanistan zimesema, msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid amesema upande wake unajadiliana na baadhi ya viongozi wa kisiasa wa Afghanistan, na masuala husika ya kuunda serikali mpya yanatarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

Siku hiyo baadhi ya viongozi wa kisiasa wa Afghanistan walisema ingawa wamekutana na upande wa Taliban, lakini hadi sasa bado hawajajadiliana kwa kina masuala ya kuunda serikali. Wakati huohuo, baadhi ya viongozi wa kisiasa wa Afghanistan wanalaumu kuwa majadiliano yanayoendelea si mapana na hayana ushirikishi.

Wiki moja imeshapita sasa tangu Taliban idhibiti Kabul, mji mkuu wa Afghanistan, na mchakato wa kuunda serikali mpya ya nchi hiyo unafuatiliwa na pande nyingi.