Rais wa China amtumia salamu za pongezi rais mteule wa Zambia
2021-08-24 10:59:30| CRI

 

 

Rais Xi Jinping wa China amemtumia salamu Hakainde Hichilema, na kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Zambia.

Kwenye salamu zake rais Xi amesema China na Zambia ni marafiki, wenzi na ndugu wakubwa, na tangu zianzishe uhusiano wa kibalozi zimeimarisha hali ya kuaminiana katika mambo ya kisiasa, na ushirikiano katika sekta mbalimbali, zaidi ya hayo zimeelewana na kuungana mkono katika masuala muhimu yanayohusisha maslahi yao makuu na zinayoyafuatilia kwa pamoja. Ameeleza kuwa anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Zambia, na kuthamini urafiki wa jadi kati ya nchi zao. Pia ameongeza kuwa anapenda kushirikiana na rais Hichilema katika kukuza ushirikiano, ili kuwanufaisha nchi hizo mbili na wananchi wao.