Bandari ya Lamu iliyojengwa na China kuwa kituo kikuu cha usafirishaji
2021-08-24 10:12:14| CRI

Bandari ya Lamu iliyojengwa na China kuwa kituo kikuu cha usafirishaji_fororder_2

Kenya itaiinua bandari ya Lamu iliyojengwa na China na kuwa kituo cha usafirishaji cha kikanda, kuchochea utengezaji wa ndani na kutoa ajira.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Kenya Ukur Yatani kwenye taarifa aliyoitoa Jumapili baada ya kufanya ziara kwenye bandari ya Lamu. Amesema bandari hiyo kubwa iliyopo kwenye Kisiwa cha Lamu, inapangwa kuwa kituo cha kusafirisha mizigo mingi inayokwenda nchi za nje, kwani ina uwezo wa kufunga gati meli kubwa zenye uwezo wa kubeba zaidi ya makontena elfu 10 yenye ukubwa wa futi 20.

Julai 15 Bandari ya Lamu ilipokea meli ya kwanza ya kibishara MV AMU1 inayomilikiwa na shirika la meli la nchi hiyo na siku chache baadaye ilipokea meli kubwa kutoka nje, na kujihakikishia nafasi yake ya kuwa kituo kikubwa cha usafirishaji katika Afrika Mashariki.