Rais Biden aweka Agosti 31 kuwa tarehe ya mwisho ya kuondoa wanajeshi nchini Afghanistan
2021-08-25 09:59:05| CRI

Habari zimesema kuwa rais wa Marekani Joe Biden ameendelea kushikikilia kuwa Agosti 31 ni tarehe ya mwisho ya wanajeshi kuondoka Afghanistan. Rais Biden pia ametaka kuwepo kwa mipango ya dharura endapo kama baadaye ataamua jeshi la Marekani libaki Afghanistan kwa muda mrefu zaidi.

Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid ametangaza kwamba Marekani inapaswa kuondoa wanajeshi wote pamoja na wakandarasi kabla ya Agosti 31.

Ikulu ya Marekani imesema kuwa hadi sasa karibu watu 21,600 wamehamishwa nchini Afghanistan ndani ya saa 24 hadi Jumanne asubuhi.