Wawakilishi wa nchi mbalimbali wa UM wasema uingiliaji wa kijeshi wa Marekani waleta maafa makubwa kwa wananchi wa Afghanistan
2021-08-25 10:01:43| CRI

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limefanya mkutano maalumu kuhusu suala la Afghanistan jana tarehe 24, ambapo wawakilishi wa China, Cuba, Venezuela na Iran wameeleza kuwa, uingiliaji wa kijeshi umeleta maafa makubwa kwa wananchi wa Afghanistan.

Mwakilishi wa kudumu wa China katika ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva na mashirika mengine ya kimataifa nchini Uswis Chen Xu amesema, Marekani inaingilia kijeshi mambo ya nchi nyingine zenye mamlaka kamili kwa kisingizio cha demokrasia na haki za binadamu, na kuzilazimisha nchi hizo ambazo historia, utamaduni na hali zao ni tofauti kupokea mfumo wa Marekani, hali ambayo inaathiri vibaya mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi. Pia ameeleza kuwa majeshi ya Marekani, Uingereza, Australia yanayohusiana na suala la ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Afghanistan ni lazima yawajibike.

Amesisitiza kuwa China siku zote inaheshimu uhuru wa mamlaka ya Afghanistan na ukamilifu wake wa ardhi, kutoingilia kati mambo ya ndani ya Afghanistan, pia inapenda kuendelea kuchangia amani na ukarabati wa nchi hiyo.