Rais Xi Jinping wa China aongea kwa njia ya simu na mwenzake wa Russia Vladimir Putin
2021-08-26 10:33:55| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana aliongea kwa njia ya simu na mwenzake wa Russia Vladimir Putin.

Kwenye mazungumzo yao, Xi amesema tangu mwanzoni mwa mwaka huu, China na Russia ziliichukulia sherehe ya kuadhimisha miaka 20 tangu nchi hizo mbili zisaini Mkataba wa ujirani mwema na ushirikiano wa kirafiki kama mwanzo mpya, ambao utahimiza uratibu wa kimkakati na ushirikiano wa kiutendaji wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.

Xi amesema nchi hizo mbili zinapaswa kutafuta njia mpya ya ushirikiano na kupanua sekta za ushirikiano. China itashirikiana na Russia juu ya utafiti na utengenezaji wa chanjo za Corona, ili kuhakikisha usalama na utulivu wa mnyororo wa ugavi wa chanjo duniani.

Xi ameongeza kuwa nchi hizo mbili zinapaswa kutumia vizuri fursa ya miaka 20 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO), na kufanya juhudi za pamoja na nchi wanachama wengine katika kulinda usalama wa kikanda na maslahi ya maendeleo.