Kenya yazidi kutoa chanjo ya COVID-19 ili kuzuia ongezeko la maambukizi ya virusi
2021-08-26 10:40:12| CRI

Mwenyekiti wa kikosi kazi cha chanjo ya COVID-19 katika Wizara ya Afya ya Kenya Bw. Willis Akhwale amesema kuwa Kenya imeongeza kutoa chanjo dhidi ya COVID-19 wakati nchi hiyo inapata dozi za ziada kutoka kwenye majukwaa mengi ili kusaidia kuzuia maambukizi.

Ameongeza kuwa lengo la kitaifa la kutoa chanjo kamili kwa asilimia 10 ya watu ifikapo mwezi Disemba litatimizwa haraka.

Naye mkuu wa Usimamizi wa Huduma za Afya katika Wizara ya Afya Bw. Joseph Sitienei amesema serikali imetumia vifaa vya kidijitali kurahisisha utoaji wa chanjo za COVID-19, na kuongeza kuwa teknolojia zinazoibukia kama vile mawingu (cloud) nambari za majibu ya haraka (QR) na uchambuzi wa data zimeimarisha ufuatiliaji wa matumizi ya chanjo mbali na kupunguza upotezaji.