CPC yatoa waraka kuhusu majukumu na mchango wake
2021-08-26 14:24:08| cri

Idara ya Uenezi ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imetoa waraka muhimu kuhusu majukumu na mchango wake.

Waraka huo unaoitwa “CPC: Majukumu na Michango yake” umesisitiza kuwa, katika miaka mia moja iliyopita, juhudi na michango yote ya Chama hicho na Wachina chini ya uongozi wake zimefuata lengo moja, ambalo ni kustawisha taifa la China.

Waraka huo umesema, kutimiza ustawi mpya wa taifa ni jukumu la kihistoria la China na Chama hicho, na CPC imetoa ahadi isiyovunjika ya kuwaletea wananchi maisha ya furaha.

Pia umeeleza kuwa, CPC inalenga kutumikia umma na siku zote kinatanguliza maslahi yao kwanza, na kinafuata mwelekeo mkuu wa maendeleo ya kijamii na kuheshimu hadhi muhimu ya umma katika kujenga historia.