China yaunga mkono kutafuta chanzo cha COVID-19 katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani
2021-08-29 12:14:22| Cri

Naibu mkurugenzi wa Kamati ya Afya ya Kitaifa ya China Bw. Zeng Yixin amesema, utafutaji wa chanzo cha COVID-19 ni suala la kisayansi, serikali ya China imekuwa ikiunga mkono kutafuta chanzo hicho kwa njia ya kisayansi tangu janga hilo liibuke, lakini inapinga kulifanya suala hilo kuwa la kisiasa, na kuwa chombo cha kuhamisha majukumu.

Bw. Zeng amesema hayo alipojibu swali kuhusu Idara ya Ujasusi ya Marekani kutangaza ripoti kuhusu utafutaji wa chanzo cha COVID-19.

Amesema ripoti hiyo ilitangazwa na idara ya ujasusi ya Marekani wala si shirika la kitaaluma la udaktari, hali ambayo imeonesha wazi nani analifanya suala la utafutaji wa chanzo cha COVID-19 liwe la kisiasa. Pia amesisitiza kuwa, hili ni suala la kisiasa ambalo linatakiwa pia ni lazima lifanyiwe uchunguzi na wanasayansi duniani kwa ushirikiano. Akitumai kuwa Marekani itaweza kutambua virusi ndio adui kwa binadamu wote, na kuchukulia utafutaji wa chanzo cha virusi kuwa suala la kisayansi, kuwahamasisha wanasayansi wa nchi mbalimbali kufanya ushirikiano kwa nguvu zote, na kuunga mkono wanasayansi kufanya utafiti kwa kina katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani.