Rais wa China asisitiza maendeleo ya sifa ya juu ya kazi ya chama cha CPC kuhusu mambo ya kikabila
2021-08-29 19:48:37| Cri

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuimarisha hisia ya jumuiya kwa taifa la China na kushughulikia mambo ya kikabila kwa kushikilia njia sahihi yenye sifa ya kichina.

Rais wa China asisitiza maendeleo ya sifa ya juu ya kazi ya chama cha CPC kuhusu mambo ya kikabila_fororder_db15a47ed93441cb8ec7b4d500c43938

Rais Xi Jinping wa China pia alitembelea Jumba la Makumbusho la Chengde tarehe 24 Agosti, ambapo alitazama maonesho ya picha za Kumbukumu ya Umoja ya Kitaifa ya Enzi ya Qing.

Rais Xi ameeleza kuwa, China ni nchi yenye makabila mbalimbali, ambayo imeundwa kuwa taifa la Wachina katika historia ndefu.

Mbele ya picha inayoonesha kurudi China kwa kabila la Waturhu wakati wa Enzi ya Qing, rais Xi ameeleza kuwa kabila la Waturhu lilidhamiria kurudi China baada ya kutenganishwa nje kwa miaka 100, hali ambayo imeonesha ushawishi mkubwa wa taifa la Wachina.

Rais Xi asifu kabila la Waturhu miaka 200 iliyopita_fororder_0829 图片1

Wilaya inayojiendesha ya Bayinguoleng ya Mongolia iliyoko kwenye Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang wanaishi warithi wengi wa kabila wa Waturhu. Kila mwaka tarehe 23 Juni, shughuli mbalimbali zinafanyika kwa ajili ya kukumbuka kurudi China kwa kabila hilo. Filamu na maonesho mbalimbali pia zimeonesha moyo wao wa uzalendo na mshikamano, pamoja na imani yao dhamira.