Wafanyabiashara zaidi 4,000 washiriki kwenye maonyesho ya biashara ya huduma ya China kwa njia ya mtandao
2021-08-30 09:13:47| CRI

Waandaaji wa maonesho ya kimataifa ya biashara ya huduma ya China (CIFTIS) wamesema makampuni 4,357 yamejiandikisha kushiriki kwenye maonyesho hayo kupitia mtandao wa internet bila shughuli zozote za nje ya mtandao.

Waandaaji wa maonesho hayo wamesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa idadi ya makampuni yatakayoshiriki imeongezeka kwa asilimia 40 kuliko mwaka jana.

Jukwaa la kidijitali la maonesho hayo litaruhusu washiriki kuonyesha bidhaa, kufanya mikutano na kusaini makubaliano. Jukwaa hilo litatoa huduma ya tafsiri ya moja kwa moja kwa washiriki kutoka nchi za nje. Maonesho hayo yatafanyika hapa Beijing kuanzia tarehe 2 hadi tarehe 7 Septemba.