Mkutano wa kazi za makabila madogo nchini China wafanyika
2021-08-30 13:06:43| CRI

Mkutano wa kazi za makabila madogo nchini China wafanyika_fororder_e86804c5672841f0add1150d04851ff3

Mkutano wa kazi za makabila madogo madogo nchini China umefanyika hapa Beijing, ambapo rais Xi Jinping wa China amesisitiza umuhimu wa kazi za makabila hayo.

Rais Xi amesema, jambo la kujivunia ni kwamba, China imepata njia sahihi na maalumu ya kutatua masuala ya makabila madogo madogo. Amesisitiza kutekeleza kwa pande zote mawazo ya Chama cha Kikomunisti cha China ya kuimarisha na kuboresha kazi za makabila madogo madogo, kukuza mawasiliano na maingiliana ya makabila mbalimbali nchini China, kuhimiza maendeleo ya sehemu za makabila madogo madogo, na kuhamasisha watu wa makabila yote kushikamana na kufanya juhudi za pamoja kwa ajili ya malengo ya maendeleo ya taifa la China.