Baadhi ya vifo vya watu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kabul vyatokana na ufyatuaji risasi wa Wamarekani
2021-08-30 13:04:24| cri

Baadhi ya vifo vya watu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kabul vyatokana na ufyatuaji risasi wa Wamarekani_fororder_1

Mashambulizi ya mabomu yaliyotokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kabul, Afghanistan yamesababisha vifo na majeruhi ya watu mia kadhaa, na baadhi ya vifo vimetokana na ufyatuaji risasi wa wanajeshi wa Marekani.

Habari zilizothibitishwa na familia za marehemu na vyombo vya habari vya Afghanistan zinasema, baadhi ya watu waliuawa na wanajeshi wa Marekani kwenye vurugu zilizotokana na milipuko ya mabomu.