Msemo huo ulianza kujulikana miaka 2,700 iliyopita nchini China, na maana yake ni kuwa kazi ni msingi wa maisha ya watu, na hutakosa nguo na chakula ukifanya kazi kwa bidii. Nadhani waswahili pia watakumbuka misemo mingi inayohamasisha kazi na kujituma, mfano mgaagaa na upwa hali wali mkavu, au mchumia juani hulia kivulini.