Wataalamu wa China na Afrika wakutana kujadili hifadhi ya wanyamapori
2021-08-31 09:21:53| CRI

Watalaamu kutoka China na Afrika wameshiriki kwenye mkutano uliofanyika kwa njia ya video kujadili njia za kivumbuzi za kuimarisha udhibiti endelevu na matumizi ya viumbe pori.

Mkutano huo umeandaliwa na Muungano wa mashirika ya kijamii ya Afrika wa kulinda viumbe anuai ACBA na Muungano wa kijamii wa China unaoshughulikia ulinzi wa viumbe anuai CSABC.

Mkutano huo umesisitiza umuhimu wa kuhifadhi viumbe anuai na kuhakikisha maisha ya kijamii ya huko. Wataalamu wa China na Afrika wamekubaliana kuwa maslahi ya afya, maendeleo ya uchumi na muungano kati ya wenyeji na jamii za huko vina uhusiano wa moja kwa moja na ulinzi wa mfumo wa kiikolojia ikiwemo misitu.